Nenda kwa yaliyomo

Tacitus

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu yake nje ya Bunge la Austria.

Publius (au Gaius) Cornelius Tacitus (56 hivi - 120 hivi BK) alikuwa mwanasiasa na mwanahistoria wa Dola la Roma.

Vitabu vyake maarufu vilivyotufikia kwa sehemu tu vinaitwa kwa Annales na Historiae. Vinasimulia historia ya dola hilo kuanzia mwaka 14 hadi 70.

Maandishi yake mengine yanahusu ufundi wa kutoa hotuba (Dialogus de oratoribus), Ujerumani (De origine et situ Germanorum), na maisha ya mkwe wake, jenerali Gnaeus Julius Agricola, aliyeteka sehemu kubwa ya Britania (De vita et moribus Iulii Agricolae).

Tacitus anahesabiwa kati ya wanahistoria bora wa Roma ya Kale.[1][2]

  1. Van Voorst, Robert E (2000). Jesus Outside the New Testament: An Introduction to the Ancient Evidence Eerdmans Publishing ISBN 0-8028-4368-9 pages 39-42
  2. Backgrounds of early Christianity by Everett Ferguson 2003 ISBN 0-8028-2221-5 page 116
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tacitus kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.