Nenda kwa yaliyomo

Stani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Stani (stannum; kiing. tin)
Vipande vya stani
Vipande vya stani
Jina la Elementi Stani (stannum; kiing. tin)
Alama Sn
Namba atomia 50
Mfululizo safu Metali
Uzani atomia 118.710
Valensi 2, 8, 18, 18, 4
Densiti 7.31 g/cm³
Ugumu (Mohs) {{{ugumu}}}
Kiwango cha kuyeyuka 505.08 K (231.93 °C)
Kiwango cha kuchemka 2875 K (2602 °C)
Asilimia za ganda la dunia 3 · 10-3 %
Hali maada mango
Mengineyo Stani kwa mazingira ya wastani ina alotropi mbili au maumbo mawili yaani stani nyeupe na stani kijivu

Stani (ing. tin) ni elementi. Namba atomia yake ni 50 kwenye mfumo radidia na uzani atomia ni 118.710. Jina ni neno la kilatini stannum kwa metali hii.

Ni metali laini sana yenye rangi ya kifedha-kijivu. Huyeyuka mapema kwenye kiwango cha halijoto cha 505 °C. Hupatikana hasa kama oksidi katika mitapo.

Matumizi ya kihistoria

[hariri | hariri chanzo]

Katika historia ilikuwa kati ya metali za kwanza zilizotumiwa na binadamu katika teknolojia. Bronzi ambayo ni aloi ya shaba na stani ilikuwa metali ya kwanza ya vifaa vya kazi na silaha katika nchi nyingi kabla ya teknolojia ya chuma. Mahitaji ya stani yalikuwa sababu muhimu kwa Waroma kuvamia Britania penye migodi muhimu ya stani katika rasi ya Cornwall.

Matumizi ya kisasa

[hariri | hariri chanzo]

Matumizi ya stani duniani ni takriban tani 300,000 kwa mwaka.

Theluthi moja ya mahitaji ni kwa ajili ya aloi za lihamu kwa kazi za kulehemia. Matumizi haya yamezidi kuwa muhimu kutokana mahitaji makubwa ya kompyuta na vifaa vya elektroniki.

Stani haioksidiki kirahisi hewani na hujiunga na chuma. Hivyo theluthi nyingine ya mahitaji ya stani ni kama koti kwa mabati ya chuma au kwa bati za kopo ni kinga dhidi ya kutu.