Nenda kwa yaliyomo

Pikomita

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uchoraji wa atomi ya heliu ambayo ina kipenyo cha pikomita 3[1]
Simple English Wiktionary
Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno:

Pikomita (ing. picometer, alama pm) ni kipimo cha SI cha kutaja urefo mdogo wa mita 10−12.

Hi ni sawa na sehemu ya milioni 1 (yaani = 1/1,000,000) ya mikromita (inayoitwa pia mikron). Zamani iliitwa "micromicron", stigma au bicron.[2] wakati ule alama yake ilikuwa µµ.[3]

Kipimo hiki hutumiwa kwa kutaja vipimo katika fizikia ya atomi na chembe zake, kemia na elimu ya sauti. Kipenyo cha atomi ni kati ya pikomita 62 hadi 520.

Neno linatokana na lugha ya Kiitalia: piccolo (kadogo).

  1. "Atomic radius". WebElements: the periodic table on the web.
  2. Deza, Elena; Deza, Michel Marie (2006). Dictionary of Distances. Elsevier. ISBN 0-444-52087-2.
  3. How Many? A Dictionary of Units of Measurement; Russ Rowlett and the University of North Carolina at Chapel Hill; http://www.unc.edu/~rowlett/units/dictB.html Ilihifadhiwa 20 Desemba 2016 kwenye Wayback Machine.