Nenda kwa yaliyomo

Ruhuhu (mto)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mto Ruhuhu)
Ruhuhu
Chanzo Milima ya Kipengere, Mkoa wa Iringa, Tanzania
Mdomo Ziwa Nyasa, upande wa kusini ya Manda (Ludewa)
Nchi Tanzania
Urefu ~300 km

Mto Ruhuhu ni mto wa Tanzania Kusini. Chanzo chake kiko katika milima ya Kipengere upande wa kusini wa Njombe ikielekea kwanza kusini-mashariki na baadaye magharibi inapoishia katika Ziwa Nyasa karibu na mji wa Manda.

Mwendo wake una urefu wa kilomita zaidi ya 300. Hivyo ni tawimto mrefu wa Ziwa Nyasa na kutokana na hali hii inahesabiwa kama chanzo cha mto Shire unaopeleka maji ya ziwa kwenda mto Zambezi na Bahari Hindi.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]