Nenda kwa yaliyomo

Msomaji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Msomaji.

Msomaji ni mtu anayesoma maandishi fulani, hasa vitabu. Kwa njia hiyo anapokea ujumbe kutoka kwa waandishi.

Katika Ukristo

[hariri | hariri chanzo]
Mimbari ya Aiello katika kanisa kuu la Salerno, Italia.
Mimbari ya Pieve di Lemine huko Almenno San Salvatore, Bergamo, Italia.
Mimbari ya Kikalvini huko Chicago, Marekani.

Katika Ukristo ni hasa jina la mtu anayesoma kutoka katika Biblia wakati wa ibada, akiwa amejiandaa kutoa huduma hiyo kwa kiwango cha ubora ili Neno la Mungu lisikike vizuri.

Katika Kanisa la Kilatini

[hariri | hariri chanzo]

Katika Kanisa la Kilatini na baadhi ya madhehebu mengine, waumini wanaweza kukabidiwa huduma hiyo kwa namna ya kudumu.

Hasa wanaojiandaa kupata ushemasi na upadri wanatakiwa kupitia kwanza usomaji na usindikizi kama matayarisho kwa daraja takatifu hizo.

Kuanzia mwaka 2021 wanawake pia wanaweza kupewa kazi hiyo, baada ya Papa Fransisko kurekebisha kanuni 230 ya Mkusanyo wa Sheria za Kanisa.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]