Mreteni
Mreteni | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mreteni mashariki (Juniperus procera)
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Spishi 67, 6 katika Afrika:
|
Mireteni ni miti yenye koni ya jenasi Juniperus katika familia Cupressaceae ya oda Pinales (mikoni) ambayo koni zao zina nyama.
Miti hiyo inasambaa kwa upana kupitia Nusudunia ya Kaskazini kutoka Aktiki kuelekea kusini mpaka Afrika ya Kaskazini, Uturuki, Pakistani, Tibet, Japani na Amerika ya Kati. Spishi moja, mreteni mashariki (Juniperus procera), inapatikana chini ya Sahara. Misitu ya mireteni juu kabisa inapatikana kwa mwinuko wa m 4900 katika kaskazini kwa Himalaya inayoumba mmoja ya mipaka ya miti ya kimo juu kabisa duniani.
Maelezo
[hariri | hariri chanzo]Ukubwa na muundo wa mireteni hutofautiana kutoka miti ya urefu wa m 20-40 hadi vichaka vilivyoenea chini na huwa na matawi marefu yanayotambaa. Huwa na majani kijani mwaka mzima na hayo yanafanana na sindano na/au magamba. Hubeba maua kwenye mti mmoja au miti tofauti. Koni za mbegu za kike ni bainifu sana zenye magamba kama matunda yaliyo na nyama na kuungana ili kuunda umbo la "beri" za urefu wa mm 4-27. “Beri” hizo huwa na mbegu 1-12 zisizo na mabawa lakini zilizo na ganda ngumu. Kwa spishi fulani "beri" ni kahawianyekundu au zina rangi ya machungwa, lakini kwa nyingi nyingine rangi ni buluu. Mara nyingi huwa na harufu nzuri na inaweza kutumika kama kiungo. Muda wa kukomaa kwa mbegu hutofautiana kati ya spishi kutoka miezi 6 hadi 18 baada ya uchavushaji. Koni za kiume ni sawa na zile za Cupressaceae ingine na huwa na magamba 6-20.
Mireteni mingi (k.m. J. Chinensis na J. virginiana) ina aina mbili za majani: miche na matawi kadhaa ya miti inayokonga yana majani kama sindano ya urefu wa mm 5-25 na majani kwenye miti iliyokomaa ni madogo sana kwa kawaida (mm 2-4), hupishana na huwa kama magamba. Majani machanga yakitokea kwenye miti iliyokomaa mara nyingi hupatikana kwenye machipukizi katika kivuli na majani mapevu kwa jua. Majani kwenye machipukizi yakuayo haraka mara nyingi ni kati ya machanga na mapevu. Kwa spishi fulani (k.m. J. Communis na J. squamata) majani yote ni ya aina ya sindano bila majani kama magamba. Kwa baadhi ya haya (k.m. J. communis) sindano zimeunganishwa chini, huku kwa nyingine (k.m. J. squamata) sindano huunganika vizuri na shina.
Majani kama sindano ya mireteni ni magumu na makali, inayofanya majani machanga kuwa kuchomachoma sana yakishughulika. Hii inaweza kuwa sifa ya kutambulisha baina ya miche, kwani majani machanga ya misanduku ingine yaliyo sawa vinginevyo ni laini na siyo kuchomachoma.
Spishi za Afrika
[hariri | hariri chanzo]- Juniperus cedrus, Mreteni wa Kanari
- Juniperus communis, Mreteni wa Ulaya
- Juniperus oxycedrus, Mreteni wa Mediteranea
- Juniperus procera, Mreteni Mashariki
- Juniperus thurifera, Mreteni wa Hispania
- Juniperus turbinata, Mreteni wa Finisia???
Spishi za mabara mengine
[hariri | hariri chanzo]- Juniperus angosturana
- Juniperus arizonica
- Juniperus ashei
- Juniperus barbadensis
- Juniperus bermudiana
- Juniperus blancoi
- Juniperus brevifolia
- Juniperus californica
- Juniperus chinensis
- Juniperus coahuilensis
- Juniperus comitana
- Juniperus convallium
- Juniperus coxii
- Juniperus davurica
- Juniperus deltoides
- Juniperus deppeana
- Juniperus drupacea
- Juniperus durangensis
- Juniperus excelsa
- Juniperus flaccida
- Juniperus foetidissima
- Juniperus formosana
- Juniperus gamboana
- Juniperus gracilios
- Juniperus grandis
- Juniperus horizontalis
- Juniperus indica
- Juniperus jaliscana
- Juniperus komarovii
- Juniperus macrocarpa
- Juniperus maderensis
- Juniperus maritima
- Juniperus martinezii
- Juniperus monosperma
- Juniperus monticola
- Juniperus morrisonicola
- Juniperus mucronata
- Juniperus navicularis
- Juniperus occidentalis
- Juniperus osteosperma
- Juniperus phoenicea
- Juniperus pinchotii
- Juniperus pingii
- Juniperus poblana
- Juniperus polycarpos
- Juniperus procumbens
- Juniperus przewalskii
- Juniperus pseudosabina
- Juniperus recurva
- Juniperus rigida
- Juniperus sabina
- Juniperus saltillensis
- Juniperus saltuaria
- Juniperus saxicola
- Juniperus scopulorum
- Juniperus semiglobosa
- Juniperus squamata
- Juniperus standleyi
- Juniperus taxifolia
- Juniperus tibetica
- Juniperus virginiana
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Mreteni wa Kanari
-
Mreteni wa Ulaya
-
Mreteni wa Mediteranea
-
Mreteni wa Finisia
-
Mreteni mashariki
-
Mreteni wa Hispania
-
Koni zenye nyama
-
California juniper
-
Chinese juniper
-
Greek juniper
-
Creeping juniper
-
Iberian juniper
-
Savin juniper
-
Spanish juniper