Mkoa wa Shinyanga
Mkoa wa Shinyanga ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye msimbo wa posta 37000. Mkoa umepakana upande wa kaskazini na mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera, upande wa kusini na Mkoa wa Tabora. Mkoa wa Kigoma uko upande wa magharibi, na mkoa wa Simiyu upande wa mashariki.
Makao makuu yako mjini Shinyanga.
Wilaya
[hariri | hariri chanzo]Mkoa wa Shinyanga una wilaya 6: Kahama Mjini, Ushetu, Msalala, Kishapu[1], Shinyanga Vijijini na Shinyanga Mjini.
Wilaya tano zimepelekwa kwenda mikoa mipya ya Simiyu na Geita.[2], [3]
Wakazi
[hariri | hariri chanzo]Baada ya kumegwa upande wa mashariki na kuzaa mkoa wa Simiyu, Shinyanga ina wakazi 2,241,299 kufuatana na sensa ya mwaka 2022[4] kutoka wakazi 1,534,808 wa sensa ya mwaka 2012.[5]
Makabila ya Shinyanga hasa ni Wasukuma, Wanyamwezi na Wasumbwa.
Wakazi wa Mkoa wa Shinyanga hujishughulisha na uchimbaji mdogo wa madini ya dhahabu na almasi. Kuna migodi mikubwa ya uchimbaji wa madini ya almasi katika mgodi wa Mwadui na dhahabu katika migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi.[6]
Mgodi wa almasi wa Williamson
[hariri | hariri chanzo]Mgodi wa Williamson Diamond, ulioko katika Mkoa wa Shinyanga kilomita 160 kusini mwa jiji la Mwanza, ni moja ya mabomu saba yanayoendeshwa na Petra Diamonds. Mgodi huo kwa 75% inamilikiwa na almasi ya Petra na 25% na Serikali ya Tanzania. Williamson ni mgodi wazi wa shimo ulioenea juu ya eneo la hekta 146. Mgodi huo umekuwa ukifanya kazi kwa miaka 70. Bado ina rasilimali muhimu ya almasi bado inapaswa kuchimbwa. Mpango wa sasa wa mgodi kwa Williamson ni kwa miaka 18. Maisha yanayowezekana ya mgodi ni zaidi ya miaka 50.
Mgodi huo umetajwa kwa jina la Dk John Williamson, mtaalamu wa jiolojia wa Canada, ambaye aligundua mnamo 1940 kama amana ya msingi ya kiuchumi ya almasi. Dk Williamson alisimamia mgodi huo hadi kifo chake mnamo 1958.[7]
Majimbo ya bunge
[hariri | hariri chanzo]Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:
- Kahama Mjini : mbunge ni Jumanne Kishimba (CCM)
- Kishapu : mbunge ni Suleiman Nchambi (CCM)
- Msalala : mbunge ni Ezekiel Maige (CCM)
- Shinyanga Mjini : mbunge ni Patrobas Katambi (CCM)
- Solwa : mbunge ni Ahmed Ally Salum (CCM)
- Ushetu : mbunge ni Elias Kwandikwa (CCM)
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ [wilaya ya Kishapu ina kata 20 nazo ni: Bubiki | Bunambiyu | Itima | Kiloleli | Kishapu | Lagana | Masanga | Mondo | Mwadui Lohumbo | Mwakipoya | Mwamalasa | Mwamashele | Ngofila | Seke-Bukoro | Shagihilu | Somagedi | Songwa | Talaga | Uchunga | Ukenyenge. https://www.wikiwand.com/sw/Wilaya_ya_Kishapu
- ↑ Bukombe imepelekwa Mkoa wa Geita.
- ↑ Wilaya za Maswa, Bariadi na Meatu zimepelekwa Mkoa wa Simiyu.
- ↑ https://www.nbs.go.tz
- ↑ Sensa ya 2012, Shinyanga Region
- ↑ http://www.shinyanga.go.tz/economic-activity/uchimbaji-wa-madini.
- ↑ https://www.mining-technology.com/projects/williamson-mine-shinyanga-province/.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Shinyanga Region Homepage for the 2002 Tanzania National Census
- Tanzanian Government Directory Database
- Shinyanga Investment profile Ilihifadhiwa 24 Oktoba 2015 kwenye Wayback Machine.
- Taarifa ya hali ya kilimo - Mkoa wa Shinyanga Ilihifadhiwa 5 Machi 2016 kwenye Wayback Machine.
Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Geita | Iringa | Kagera | Katavi | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Njombe | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Simiyu | Singida | Songwe | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Shinyanga bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mkoa wa Shinyanga kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |