Tofali
Tofali ni nyenzo inayotumiwa katika ujenzi wa majengo. Kimsingi ni kama jiwe linalotengenezwa na binadamu kutokana na udongo unaofaa hasahasa udongo kinamo.
Matofali hutengenenzwa kwa kutumia udongo unaopatikana ambao huchanganywa na maji ili kuweza kushikamanisha udongo huo ili kupokea umbo linalotakiwa.
Udongo unaofaa
[hariri | hariri chanzo]Hivyo tofali hupatikana pale ambapo udongo kinamo unapatikana uliofanywa na punje ndogo za mchanga (kipenyo cha milimita 0,063 hadi 1) pamoja na punje ndogo zaidi za minerali (milimita 0,0002 hadi 0,063) ndani yake lakini isiyo na mata ogania. Udongo kinamo unaweza kushika maji ndani yake na hivyo kuwa na tabia ya plastiki yaani inakubali kubadilishwa maaumbo mbalimbali. Kama udongo kinamo una pande ndogo sana pekee ni udongo wa mfinyanzi lakini kwa matumizi ya matofali si lazima kuwa laini vile. Kama punje ndani yake ni kubwa zaidi tofali haiwezi kuwa imara sana.
Baada ya kukauka tofali imepotea maji ndani yake na kuwa ndogo zaidi; ikipashwa moto punje ndani yake zinashikana na kuwa imara zaidi.
Udongo wote unaweza kuchanganywa na saruji na kuwa imara kwa kukauka tu ilhali ni saruji inaleta uimara kazi ya punje za udongo.
Uandaaji wa tofali
[hariri | hariri chanzo]Kabla ya kuitwa tofali kitu cha kwanza ni kutafuta mchanga ususani kwa matofali ya simenti lakini kwa matofali ya udongo huwa ni kwanza kutafuta udongo mzuri kwa ajiri ya kushikamanisha na maji baadae. Kwa udongo wa mfinyanzi ni mzuri kuliko udongo mwingine kwa kutengeneza tofali la udongo. Lakini pia kwa matofali ya kuchoma huhitaji udongo mzuri pia unao shikamana kwa ajili ya kutangeneza tofali. Baada ya kutafuta udongo mzuri zoezi la uchanganyaji wa maji huanza kwa aina zote za matofali. Mara nyingi utengenezaji wa matofali huhitaji fremu ya kibao kwa ajili ya kuandaa muundo maalumu wa tofali lenyewe maalumu kwa ajili ya ujenzi wa nyumba.
Katika nchi mbalimbali kuna uzoefu wa kuchanganya udongo na ubua (manyasi makavu) ndani yake; hii inasaidia kushikana tofali kwa ndani na kupunguza uzito.[1]
Aina za matofali
[hariri | hariri chanzo]kuna aina mbalimbali za matofali kutokana na udongo au mchanga unaotumika kutengeneza tofali lenyewe. Aina hizo zinazotokana na udongo au mchanga ni kama zifuatazo
- Tofali la udongo uliokauka
- Tofali la kuchoma
- Tofali la block
Tofali bichi
[hariri | hariri chanzo]Makala kuu:Tofali bichi
Hili ni tofali linalopatikana baada ya kuchanganya udongo mzuri ambao unashikamana vizuri na baada ya hapo udongo huchanganywa na maji ili kuweza kushikamana vizuri na baadae udongo huwekwa kwenye kalibu maalumu ilikutoa tofali husika. Matofali haya yanaweza kudumu kama yanatumiwa katika maeneo penye mvua kidogo. Lakini yakiloweshwa mara nyingi au kwa muda mrefu hupokea maji tena na kupoteza umbo. Inawezekana pia kufunika ukuta wa matofali yaliyokauka kwa lipu. Katika mazingira yabisi sana au jangwani majengo ya matofali mabichi yamedumu karne kadhaa. Tofali bichi ni tofali lenye uwezo mkubwa wa kuhimili majanga.
Tofali la kuchoma
[hariri | hariri chanzo]Hili ni tofali linalopatikana baada ya kutengeneza tofali la udongo na kulichoma kwa kutumia moto. Tanuri ya matofali unafunikwa kwa gana la udongo nje na chini yake moto inawaka kwa siku 2 au 3. Kutengeneza matoli wa njia hii ina gharama zaidi laini matofali yaliyochomwa hudumu zaidi hata penye mvua. Kiasi jinsi udongo mzuiri inapashwa moto zaidi matofali hutoka magumu na bora zaidi.
Tofali la block
[hariri | hariri chanzo]Hili ni tofali linalopatikana baada ya kutumia mchanga pamoja na kuchanganya na simenti tofali hili huwa ni tofali imara kupita matofali yaliyokauka na huweza kujenga nyumba imara sana. Uimara na gharama hutegemea na kiwango cha simenti inayotumiwa. ililiwe tofali
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Linganisha taarifa ya Biblia katika kitabu cha Kutoka 5,6f: Waebrania walipaswa kutafuta manyasi makavu " Farao akawaamuru wasimamizi wa watu.. akisema, 5:7 Msiwape watu tena majani ya kufanyia matofali, kama mlivyofanya tangu hapo; na waende wakatafute majani wenyewe. "
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- media kuhusu Matofali (bricks) pa Wikimedia Commons
- "Bricks Made Automatically by One-Man Machine" Popular Mechanics, April 1935, pg. 523 bottom-left
- Jonathan Ochshorn:Brick in 20th-Century Architecture, Encyclopedia of Twentieth Century Architecture, Fitzroy Dearborn (Taylor and Francis) Publishers 2003