Kinyama-kigoga
Kinyama-kigoga | ||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||
| ||||||||
Ngazi za chini | ||||||||
Ngeli 3, oda 4:
|
Vinyama-kigoga (tafsiri la jina la kisayansi) ni wanyama wadogo wa maji matamu na ya chumvi wa faila Bryozoa. Ni wanyama sahili na karibu wote huishi katika makoloni yanayoshikamanisha kwenye nyuso mbalimbali, kama vile miamba, mawe, mchanga, makombe na miani. Kwa kawaida wana urefu wa takriban mm 0.5 na wana muundo maalum wa kujilisha unaoitwa lofofori (lophophore), "taji" ya minyiri inayotumiwa kwa kujilisha kwa njia ya kuchuja. Spishi nyingi za baharini huishi katika maji ya kitropiki, lakini kadhaa hupatikana katika mifereji ya bahari na maji ya maeneo ya ncha za dunia. Vinyama-kigoga wameainishwa kama spishi za baharini (Stenolaemata), spishi za maji tamu (Phylactolaemata) na spishi za baharini na pengine maji ya chumvi kidogo (Gymnolaemata). Spishi hai 5,869 zinajulikana[1]. Spishi za jenasi moja huishi peke yao, nyingine zote huishi katika makoloni.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Bock, P.; Gordon, D.P. (Agosti 2013). "Phylum Bryozoa Ehrenberg, 1831". Zootaxa. 3703 (1): 67–74. doi:10.11646/zootaxa.3703.1.14.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)