Nenda kwa yaliyomo

Karelia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sehemu ya mkoa wa Karelia.
Mahali pa Karelia katika Russia.

Karelia ni mkoa ulioko nchini Urusi.

Mji mkuu wake ni Petrozavodsk.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Karelia ilikaliwa na wakazi wanaoongea Kifini. Kwa muda mrefu maeneo yake yaligombaniwa baina ya Urusi na Uswidi.

Tangu mwaka 1721 sehemu kubwa ya Karelia ilikuwa sehemu ya Milki ya Urusi, sehemu nyingine ilibaki upande wa Uswidi ikawa baadaye sehemu ya ufalme mdogo wa Ufini ndani ya milki ya Urusi.

Baada ya uhuru wa Ufini mnamo 1918, Wakarelia walijikuta katika nchi mbili tofauti. Baada ya Vita ya Umoja wa Kisovyeti dhidi ya Finland, sehemu kubwa ya Karelia ya Ufini ilihamishwa upande wa Urusi.

Umoja wa Kisovyeti ilipeleka Warusi na Waukraina wengi Karelia, hivyo asilimia ya watu wanaoendelea kusema Kifini imepungua sana.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu maeneo ya Urusi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Karelia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.