Nenda kwa yaliyomo

Johann van der Sandt

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Johann van der Sandt, ni mwanamuziki wa Afrika Kusini ambaye alizaliwa katika jimbo la Dola Huru . Alisoma katika Chuo Kikuu cha Pretoria [1] ambapo alipata B. Mus (Ed), B. Mus (Hons), M Mus (Musiekwetenskap) na D Mus (Uendeshaji wa Kwaya), pamoja na stashahada katika elimu ya Muziki ya piano, vyombo vya sauti na clarinet.

Mnamo Januari 1996 alipata stashahada ya Uendeshaji katika taasisi ya Mafunzo ya Waongoza Kwaya, Gorinchem (Uholanzi) chini ya uongozi wa Joop Schets. [2]

Van der Sandt alishikilia wadhifa kama Profesa wa Uendeshaji wa kwaya katika Chuo Kikuu cha Pretoria na alikuwa mwendeshaji rasmi wa Kwaya wa Chuo Kikuu ambapo alitekeleza mtindo wa kipekee wa uimbaji wa kwaya kwenye kampasi za Chuo Kikuu cha Afrika Kusini hadi Juni 2008.[3]

Pia alikuwa mwanzilishi wa Kwaya ya Singkronies Chamber . Lengo la kwaya ni kuunda jukwaa la kazi za watunzi wa Afrika Kusini. Kwaya iyo ilipokea Tuzo mbili za Muziki za Afrika Kusini katika kitengo cha Utendaji Bora wa Kwaya. Mnamo 2006 Van der Sandt aliweka pamoja Can't'Afrika, kikundi cha uimbaji cha waimbaji 12 ambao lengo lao ni kusoma na kufanya kazi za watunzi wa Afrika Kusini.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
  1. "Johannes Theodorus van der Sandt". www.unibz.it (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2021-08-25.
  2. "Johannes Theodorus van der Sandt". www.unibz.it (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2021-08-25."Johannes Theodorus van der Sandt". www.unibz.it
  3. https://www.unibz.it/en/faculties/education/academic-staff/person/35788-johannes-theodorus-van-der-sandt
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Johann van der Sandt kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.