Nenda kwa yaliyomo

Grace Gao (mwanaharakati)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Grace Gao

Grace Gao (anajulikana pia kama Grace Geng[1]; amezaliwa 1993) ni mwanaharakati wa haki za binadamu nchini Uchina. Yeye ni binti Gao Zhisheng, wakili wa Kichina wa haki za binadamu na mpinga sera za serikali.[2] Yeye na familia yake wamepelelezwa, kupigwa, na kutishwa na mamlaka za Uchina.[2] Anaelimisha kimataifa ili kutangaza kitabu cha baba yake A China More Just na kutilia mkazo kwenye kesi yake (kwa sasa, ametoweka na mamlaka za Uchina zinahusika na kutoweka kwake[3]), na kusema dhidi ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Uchina.[2] "Kwa hiyo, ninajikuta katika nafasi ya kuchukua vazi hilo na kuwa mtetezi wa haki za binadamu kama baba yangu... Ukweli ni nguvu na nitaendelea kuongea mpaka baba yangu awe huru".[4][5]

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Gao alikuwa akisindikizwa kwenda shuleni kila siku na maafisa wa polisi ambao walimfuata kila alikoenda.[2] Grace alijijeruhiwa kwa sababu ya huzuni na maumivu[6] na, akiwa na umri wa miaka 17, alijaribu kujiua mara kadhaa. Alipata ugumu kuelewa maamuzi ya baba yake.

Baada ya Gao kuzuiwa na serikali kuhudhuria shule,[2] mama yake aliamua kuwasafirisha yeye pamoja na kaka yake (Peter, b. 2005) kutoka Uchina.[2] Mnamo tarehe 9 Januari 2009, walikimbilia Uthai kwa usafiri wa pikipiki na basi (wakiwa wamejificha kwenye sehemu ya kubeba mizigo),[7] kisha wakaenda Merika ambako walipewa hifadhi ya kisiasa.[7][8] Huko New York, Grace alipata matibabu hospitalini kwa miezi sita kwa maswala ya afya ya akili lakini bado ilikua ngumu kuamini watu. Alijifunza kumwelewa baba yake[7] na kumsaidia.

Grace alijifunza Kiingereza baada ya kuhamia Merika, alihitimu shule ya upili akiwa na miaka 20,[7] na kuendelea kusoma uchumi katika chuo kikuu cha California.

  1. "Grace Geng: Chinese dissident's daughter proud of her 'brave' father", BBC News (kwa Kiingereza (Uingereza)), 2016-06-14, iliwekwa mnamo 2021-09-16
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 2.5 "Grace Gao | Speakers | Oslo Freedom Forum". web.archive.org. 2017-08-15. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-08-15. Iliwekwa mnamo 2021-09-16.
  3. "A year on, lawyer's disappearance highlights China's escalating human rights disaster". Hong Kong Free Press HKFP (kwa Kiingereza (Uingereza)). 2018-08-13. Iliwekwa mnamo 2021-09-16.
  4. Av Hanne Mauno. "– Jeg var sjokkert. Men jeg har vokst opp i et Kina som hjernevasket meg". Dagsavisen (kwa Kinorwe). Iliwekwa mnamo 2021-09-16.
  5. Grace Geng, 'Truth is power and I will keep speaking it until my father is free'(03/10/16) for International Service for Human Rights Ilihifadhiwa 25 Juni 2021 kwenye Wayback Machine. Iliwekwa mnamo 2021-09-16
  6. "'My Father Never Spoke About The Persecution He Suffered'". Radio Free Asia (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-09-16.
  7. 7.0 7.1 7.2 7.3 "A Hero's Daughter". National Review (kwa American English). 2017-06-25. Iliwekwa mnamo 2021-09-16.
  8. hermesauto (2016-06-14). "China rights lawyer Gao Zhisheng ready for consequences over new book: Daughter". The Straits Times (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-09-16.