Nenda kwa yaliyomo

Gabi Le Roux

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Gabriel Le Roux, ni mpiga kinanda wa Afrika Kusini, mtunzi na mtayarishaji wa muziki. Amejifunza upigaji wa kinanda na jazi, ametayarisha platinum (Orodha ya vyeti vya kurekodi muziki) rekodi za muziki wa rock na Kiafrikana,[1] lakini anafahamika zaidi kwa kutengeneza muziki wa kwaito akiwa na wasanii kama Mandoza, Lebo Mathosa na TKZee.[2] Kazi yake maarufu na inayouzwa zaidi ni Nkalakatha, iliyotolewa mnamo mwaka 2000, ambayo alitayarisha Mandoza. Wimbo huo ulishika nafasi ya kwanza kwenye chati, na albamu iliyopewa jina lilelile ikaenda platinamu, ikauza zaidi ya nakala 350,000.[3]

Le Roux alianza kazi yake ya muziki kama mpiga kinanda kabla ya kuhamia katika utayarishaji, akianza na rekodi ya mbaqanga aliyotengeneza na Themba Ngwenya mnamo mwaka 1989.[2] Alianzisha studio ya kurekodi ya Kaleidosound na Tim White huko Cape Town mnamo mwaka 1995.[4] Kazi yake imepata Tuzo tano za Muziki za Afrika Kusini, zikiwemo tuzo mbili za Wimbo Bora wa Mwaka wa SAMA.[4][5]

Alikuwa mada ya sehemu kamili ya mfululizo wa filamu ya The Producers, inayoonyeshwa na M-Net kwenye chaneli ya Mzansi Magic.[6]

  1. "Gabi Le Roux". Discogs. Iliwekwa mnamo 24 Oktoba 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 "Gabi le Roux Bio". Music in Africa. Iliwekwa mnamo 24 Oktoba 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Herimbi, Helen (18 Septemba 2016). "Unifying 'Nkalakatha' Mandoza's lasting legacy". iol.co.za. Independent Online. Iliwekwa mnamo 30 Oktoba 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. 4.0 4.1 "Business profile of Gabriel (Gabi) Le Roux". Music2Deal. Iliwekwa mnamo 24 Oktoba 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Madibogo, Julia. "Artists sign petition to force Samro to pay". Citypress (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-06-15.
  6. "Mzansi Magic Interveiws Gabi Le Roux". The Producers. https://www.youtube.com/watch?v=IdG8u9B4HIA. Season 2015.