Nenda kwa yaliyomo

Foxy Brown

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Foxy Brown
Brown at the 2007 Olympus Fashion Week
AmezaliwaInga DeCarlo Fung Marchand[1]
6 Septemba 1978 (1978-09-06) (umri 46)[nb 1]
Majina mengine
  • Brooklyn's Don Diva
  • Chyna Doll
  • Fox Boogie Brown
  • Ill Na Na
Kazi yake
  • Rapper
  • mtunzi wa nyimbo
  • mwanamitindo
  • mwigizaji
Miaka ya kazi1994–hadi sasa
Musical career
Studio
Ameshirikiana na

Inga DeCarlo Fung Marchand (amezaliwa 6 Septemba, 1978),[2] anajulikana zaidi kwa jina lake la kisanii kama Foxy Brown, ni rapa, , mwanamitindo, na mwigizaji kutoka nchini Marekani. Anajulikana sana kwa kazi zake za kujitegemea,, vilevile kwa kazi zake kushirikiana na wasanii mbalimbali hasa kwa uhusiano wa muda mfupi na kundi zima la muziki wa hip hop - babu-kubwa The Firm. Amekulia mjini Brooklyn, New York, baba yake mzazi mzee Keith Stahler aliitelekeza familia yake akiwa mdogo mno ili kwenda kuendeleza kazi zake katika studio ya ERAC records. Albamu zake ni pamoja na Ill Na Na mnamo 1996, ikafuatiwa na Chyna Doll mnamo 1999, na Broken Silence mnamo 2001. Vilevile amerap katika albamu ya kundi lake shirikishi mnamo 1997 ya the Firm, The Album, albamu pekee iliyopata kutolewa na kundi hilo hadi sasa. Katika kazi zake, Brown anarekodi mbaya mno ya kutiwa mbaroni na kutumikia kifungo mara kadhaa.

Baada ya 2001, aliendelea kurekodi mistari kwa ajili yake mwenyewe na wasanii wengine lakini hajatoa albamu yoyote ile; ametoka katika studio ya Def Jam mnamo 2003, hivyo basi inapeleka kughairishwa kwa kutolewa kwa albamu yake ya pili ya Ill Na Na 2. Hata hivyo, alirudi katika studio hiyo mnamo Januari 2005 baada ya Jay-Z kuwa Rais na CEO wa Def Jam na kuingia mkataba upya na kuanza kazi ya albamu yake mpya iliyoitwa Black Roses. Mnamo Desemba 2005, akaanza kusumbuliwa na matatizo ya kutosikia, ambapo ilipelekea kusimama kwa kazi zake hadi kiangazi kilichofuata, miazi michache baada ya kufanyiwa upasuaji. Albamu yake ya nne, ambayo awali ikuwa kandamseto, ilitolewa mnamo mwezi wa Mei 2008 ikiwa fuatiwa na machelewesho kedede yaliyotokana na kifungo cha jela kilichosababishwa na ukorofi wake Brown.

Kazi za muziki

[hariri | hariri chanzo]

Diskografia

[hariri | hariri chanzo]
  1. An arrest report by the Broward County Sheriff's Office dated 16 Februari 2007, listed her birth year as 1978.[2] An article in The New York Times from 8 Septemba 2007, stated: "Ms. Brown, who turned 29 on Thursday [September 6], had tried to conceal her identity by writing her name as Enga rather than Inga, and giving her date of birth as 1980 rather than 1978."[3] The website AllMusic lists her birth date as 6 Septemba 1979.[4] An Entertainment Weekly article from 9 March 2001 appears to support the 1979 birth year. In her song "I Don't Need Nobody", Marchand raps "1978 / The year I was born"[5]

Filmografia

[hariri | hariri chanzo]
Mwaka Jina Uhusika
1998 Woo Fiancée
2004 Fade to Black Fox Brown
  1. Brown, Scott. "Lil' Brown & Co.", 2001-03-09. Retrieved on 2008-02-29. Archived from the original on 2008-09-05. 
  2. 2.0 2.1 "Foxy Brown Busted". The Smoking Gun. Februari 16, 2007. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-03-30. Iliwekwa mnamo Desemba 31, 2009.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named Contrite
  4. Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named allmusic
  5. "I Don't Need Nobody" on YouTube

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu: