Nenda kwa yaliyomo

Chuo Kikuu cha Makerere

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Makerere University
Chuo Kikuu cha Makerere
WitoWe Build for the Future
Kimeanzishwa1922
Ainaumma
ChanselaEzra Suruma
MahaliKampala, Uganda
Kampasimjini Kampala
Tovutihttp://www.mak.ac.ug
Chuo Kikuu cha Makerere

Chuo Kikuu cha Makerere ni chuo kikuu cha kwanza cha Afrika ya Mashariki na chuo kikuu kikubwa cha Uganda.

Kimeanzishwa wakati wa ukoloni mwaka 1922 kama shule ya ufundi kwa wanafunzi 14. Kozi za kwanza zilikuwa pamoja na useremala, ujenzi na umekanika.

Shule ikawa chuo na kozi zikaongezeka kwa masomo ya utabibu, kilimo, maradhi ya wanyama na ualimu.

Kuanzia mwaka 1937 chuo kilianza kozi za stashahada mbalimbali.

Mwaka 1949 Makerere ikawa chuo kishiriki cha Chuo Kikuu cha London kikitoa shahada ya kwanza ya ngazi ya chuo kikuu.

Mwaka 1963 ikawa sehemu ya Chuo Kikuu cha Afrika ya Mashariki pamoja na kampasi za Dar es Salaam na Nairobi.

Chuo Kikuu cha Afrika ya Mashariki kimegawiwa mwaka 1970 kutokana na kufifia kwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. Makerere ikawa Chuo Kikuu cha kitaifa cha Uganda.

Chuo cha Viongozi

Makerere ilikuwa chuo waliposoma viongozi wengi wa Afrika, wakiwa pamoja na marais wa zamani Milton Obote (Uganda), Julius Nyerere na Benjamin Mkapa (Tanzania) na Mwai Kibaki (Kenya).

Baada ya uhuru Makerere ilikuwa pia mahali pa majadiliano na mafunzo ya utamaduni wa Kiafrika. Waandishi na walimu muhimu wa Kiafrika walianzisha mafunzo yao au walifundisha kwa muda fulani Makerere kama vile Nuruddin Farrah, Ali Mazrui, David Rubadiri, Okello Oculi, Ngugi wa Thiongo, John Ruganda, Paul Theroux na Peter Nazareth.

Idara

Makerere ina idara 22 zinazohudumia wanafunzi 30,000 hivi, wakiwemo 3,000 wa kozi za shahada za ngazi ya juu.

Vitivo

  • Kitivo cha Kilimo
  • Kitivo cha Fani
  • Kitivo cha Elimu Misitu na Hifadhi la Mazingira
  • Kitivo cha Sheria
  • Kitivo cha Uganga
  • Kitivo cha Sayansi
  • Kitivo cha Sayansi Jamii
  • Kitivo cha Teknolojia
  • Kitivo cha Elimu ya Maradhi ya Wanyama

Taasisi

  • Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima
  • Taasisi ya Sayansi ya Kompyuta
  • Taasisi ya Uchumi
  • Taasisi ya Mazingira na Mali Asili
  • Taasisi ya Uchunguzi wa Kijamii
  • Taasisi ya Takwimu na Saikolojia

Vyuo

  • Chuo cha Ualimu
  • Chuo cha Sanaa
  • Chuo cha Sayansi za Maktaba na Habari
  • Chuo cha Biashara
  • Chuo cha Mafunzo baada ya Digrii ya Kwanza

Idara

  • Idara ya Teknolojia ya Kompyuta na Habari

Kampasi

  • Makerere - Kikara
  • Makerere - Kabanyoro
  • Makerere - Katumani

Wanafunzi waliopitia Chuo Kikuu cha Makerere

Viungo vya nje