Bandari
Bandari ni mahali pa kupokea meli na kuhamisha mizigo yao pamoja na abiria. Bandari inatakiwa kuipa meli kinga dhidi ya mawimbi makubwa na vifaa ya kupakiza au kutoa mizigo. Kuna bandari asilia na bandari zilizotengenezwa kwa kusudi hii. Kwa jumla bandari ni sehemu muhimu za miundombinu wa nchi.
Bandari hutengenezwa kando ya bahari, maziwa au mito.
Kati ya sifa muhimu kwa ajili ya bandari ni
- kina cha maji cha kutosha kulingana na ukubwa wa meli zinazoitumia.
- mitambo kama winchi za upakizi
- nafasi za ghala
- njia za usafiri kama reli na barabara za kusafirisha mizigo
Bandari hutofautiana kulingana na kusudi lao na aina za mizigo inayoshughulikiwa humo.
Bandari ndogo zinahudumia wavuvi au jahazi za burudani.
Kuna bandari zinazopokea mizigo ya kila aina kama bandari ya Dar es Salaam au Mombasa.
Mara nyingi kuna bandari zinazoshughulikia mizigo maalumu kama mafuta, kontena, kivuko na kadhalika.
Bandari zinazoshughulikia mizigo mingi duniani
(mizigo kwa mwaka tani milioni)
- Shanghai (Jamhuri ya Watu wa China) 537,0
- Singapur 448,2
- Rotterdam (Uholanzi) 378,2
- Ningbo (Jamhuri ya Watu wa China) 300,0
- Guangzhou (Jamhuri ya Watu wa China) 300,0
- Tianjin (Jamhuri ya Watu wa China) 255,0
- Hong Kong (Jamhuri ya Watu wa China) 238,0
- Nagoya (Japani) 206,0
- Qingdao (Jamhuri ya Watu wa China) 200,0
- Dalian (Jamhuri ya Watu wa China) 200,0
- Antwerpen (Ubelgiji) 167,4
- Los Angeles (USA) 162,1 (2005)
- Durban (RSA) 104,8
- Mombasa (EACU) 100,2
- Port Suez (Misri) 80,2
- Abidjan (Cote d'Ivoire) 50,6
Bandari zinazoshughulika na mizigo, bandari huru na usafiri duniani
AS
AF
AM
EU
LA
ME
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Bandari kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |