Aung San Suu Kyi
| |
Bunge la | Myanmar (Burma) |
Tarehe ya kuzaliwa | 19 Juni 1945 |
Mahali pa kuzaliwa | Rangoon (Myanmar) |
Chama | Mwenyekiti wa National League for Democracy (NLD) |
Tar. ya kuingia bunge | alishinda uchaguzi huru wa 1990 lakini amezuliwa na serikali ya kijeshi asiwe waziri mkuu |
Mengine | amefungwa ndani ya nyumba yake tangi 1990; amepewa Tuzo ya Nobel ya Amani 1991 |
Aung San Suu Kyi ni kiongozi wa harakati ya kidemokrasia nchini Myanmar (Burma) aliyefungwa ndani ya nyumba yake na serikali ya kijeshi baada ya kushinda uchaguzi huru wa mwaka 1990.
Aung San Suu Kyi amelizaliwa binti wa jenerali Aung San aliyekuwa kiongozi wa uhuru wa Burma kutoka ukoloni wa Uingereza baada ya vita vikuu vya pili vya dunia.
Alisoma chuo kikuu huko Uingereza, akaolewa na Mwingereza Michael Aris mwaka 1972 na akazaa wana wawili.
1988 alirudi Burma kumwona mamake mzee aliyekuwa mgonjwa akajikuta katika siku za mwisho za serikali ya dikteta ya kijeshi jenerali Ne Win.
Aung San Suu Kyi kama binti wa shujaa wa uhuru alikaribishwa na kujiunga na chama kipya cha upinzani akawa mwenyekiti wa National League for Democracy (NLD) iliyoshinda uchaguzi wa mwaka 1990. Serikali ya kijeshi ilibatilisha uchaguzi huu na kupiga NLD marufuku. Suu Kyi alifungwa ndani ya nyumba yake.
1991 alipewa Tuzo ya Nobel ya Amani iliyopokelewa na wanawe kwa niaba yake kwa sababu Suu Kyi aliogopa kutoka nje ya Myanmar kwa hofu hataruhusiwa kurudi tena.
Tangu zamani ile amebaki Myanmar na muda mkubwa alifungwa ndani ya nyumba yake.
Wakati wa maandamano ya wamonaki Wabuddha katika Septemba 2007 alionekana mara ya kwanza mbele ya umati wa watu lakini hakuwa na nafasi ya kuwahutubia wananchi.
Mnamo tarehe 13 Oktoba mwaka 2010, Aung San Suu Kyi aliachiliwa huru na serikali ya Myanmar baada ya kipindi chake cha kufungwa jela kuisha.