Nenda kwa yaliyomo

Angela Black

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Angela Black
Amezaliwa Angela Black

Jacksonville,Florida
Nchi Marekani
Kazi yake Mwandishi wa habari

Angela Black ni mwandishi wa habari za runinga Marekani akijulikana kwa kazi yake kwenye kituo cha KABC-TV Los Angeles, California kwenye miaka ya 1970 na 80. Black ni mmoja wa Wamarekani Weusi wa kwanza waliobobea kama watangazaji wa runinga katika eneo la Los Angeles.

Alizaliwa Jacksonville, Florida akiwa mtoto wa meja Bennie L. Canty na mwalimu Bess Canty. Wakati wa utoto wake Black aliishi katika kambi za jeshi huko Alaska na Virginia halafu familia ikahamia Jacksonville, Florida. Baada ya kuhitimu katika shule ya kikatoliki aliendelea kusoma Nashville, Tennessee kwenye Chuo kikuu cha Vanderbilt na kuhitimu katika chuo kikuu cha Jacksonville University akipata shahada ya kwanza katika Kiingereza.

Black aliajiriwa na kituo cha runinga cha KABC-TV alipohudumia kwa miaka 12 . Kazi yake ya kimsingi ilikuwa ni kuripoti matukio kutokea yanapojiri pamoja na kuwa mwandishi msaidizi siku za wikiendi akisaidiana na Jerry Dunphy kwenye usiku wa majuma. Alikuwa pia kwene timu ya Eyewitness News mwishoni mwa miaka ya 1970 na 1980.[1]

Black alihamia baadaye kwa kituo cha KCBS-TV huko Los Angeles, California, na kampuni kubwa kama HLN (TV network), PBS, na Turner Entertainment.

  1. writers, Times staff. "Journalist Files Lawsuit Against KCBS", Los Angeles Times, 2002-06-10. (en-US) 

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Angela Black kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.