Agna motto
Agnamotto ni aina ya kiungo ambayo huleta ladha katika chakula, kwa mfano nyama, maharage na hata wali.
Tunaanza kuielezea mboga yetu ambayo ni nyama: kwanza kabisa unakatakata nyama yako, ukimaliza unaiosha mara mbili; ukishamaliza unachukua tangawizi halafu unakunia kwenye nyama, ukishakunia unakunia na kitunguu saumu, unaweka chumvi yako hivyohivyo mbichi, unaweka mafuta na baada ya hapo unaikoroga mpaka ilainike. Inatumia kama dakika tano: ikishalainika unawasha moto au gesi yako. Baada ya hapo unaibandika ile nyama kwenye jiko na unaacha inachemka. Ikishachemka unaweka kitunguu na pilipili hoho. Baada ya hapo unakoroga tena, halafu unaweka nyanya, ila nyanya zako ziwe zimesagwa. Sasa unaacha zichemke kama dakika mbili huku unakoroga. Zikishachemka unaweka agnamotto yako huku nyama inachemka; baada ya hapo unaandaa chombo safi cha kuifadhia mboga yetu, sasa hivyo ndivyo agnamotto yetu inavyotumika na hapo mboga yako inakuwa ina ladha nzuri na ipo tayari kwa kuliwa.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Agna motto kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |