Abati
Mandhari
Abati (pia "abate") ni cheo cha mkuu wa monasteri yenye wamonaki wengiwengi (kwa kawaida 12 na zaidi) hasa katika Kanisa Katoliki.
Jina linatokana na Kilatini abbas, mkoko kutoka Kiaramu אבא (Abba, yaani "baba"). Kiongozi wa monasteri ya kike anaitwa pengine abesi.
Nchini Tanzania Wabenedikto wana maabati katima monasteri za Peramiho, Ndanda, Hanga na Mvimwa.
Maabati wachache wanapewa daraja takatifu ya askofu kwa kuwa monasteri yao ina jukumu la uchungaji kwa waamini wa eneo fulani (abasia ya kijimbo), kama ilivyokuwa kwa wale wa Peramiho na Ndanda wakati wa umisionari.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Russian Orthodox Abbot of Valaam Monastery
- The Pilgrimage of the Russian Abbot Daniel in the Holy Land Archived 9 Juni 2007 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Abati kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |