Nenda kwa yaliyomo

Tuvalu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Tsavorite

Tuvalu
Wito: Tuvalu mo te Atua (Kituvalu)
"Tuvalu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu"
Wimbo wa taifa: Tuvalu mo te Atua
Location of Tuvalu
Mji Mkuu
Vaiaku (kijiji),
Fongafale (kisiwa), Funafuti (atolli)
8°31′S 179°13′E / 8.517°S 179.217°E / -8.517; 179.217
Mji mkubwa --
Official languages Kituvalu, Kiingereza
Government Ufalme wa kikatiba
Independence
 -  Maji (%) (kidogo sana)
Idadi ya watu
 -  2017 Sensa 11,192
Pato la Taifa PPP makisio 2001 
 -  Jumla $12.2 million (ya 228)
 -  Per capita $1,100 (2000 est.) (unranked)
HDI (2003)0.641
medium ·n/a
Currency Dollar ya Tuvalu
Dollar ya Australia (AUD)
Saa za eneo (UTC+12)
Calling code 688
Internet TLD .tv

Tuvalu ni nchi ya visiwa katika eneo la Polynesia ya Oceania katika Bahari ya Pasifiki, takriban katikati ya Hawaii na Australia. Inapatikana mashariki-kaskazini mwa Visiwa vya Santa Cruz (ambavyo vinamilikiwa na Visiwa vya Solomon), kaskazini-mashariki mwa Vanuatu, kusini-mashariki mwa Nauru, kusini mwa Kiribati, magharibi mwa Tokelau, kaskazini-magharibi mwa Samoa na Wallis na Futuna, na kaskazini mwa Fiji.


Jina la Tuvalu lamaanisha "visiwa vinane" kwa sababu kiasili kulikuwa na visiwa 8 tu vilivyokaliwa na watu. Kisiwa cha tisa kimepata wakazi tangu mwaka 1943.

Ramani ya Tuvalu

Eneo lake ni visiwa vinne na atolli tano; kwa jumla eneo lina 26 km².

Kati ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa Tuvalu ni nchi yenye wakazi wachache kabisa.

Tuvalu ina visiwa (na atolli) vifuatavyo:

Nchi itakayopotea karibuni

[hariri | hariri chanzo]

Kama nchi mbalimbali za visiwani Tuvalu iko katika hatari ya kupotea katika miaka 50 inayokuja. Kimo cha juu cha visiwa vyake ni mita 5 pekee juu ya UB. Kubadilika kwa hali ya hewa duniani na kupanda kwa uwiano wa bahari kutamaanisha ya kwamba sehemu kubwa sana la eneo lake litazama polepole chini ya maji.

Serikali imeshaomba majirani wakubwa kama Australia na New Zealand kuwapokea wenyeji wake.

New Zealand imekubali na kwa sasa kila mwaka watu 75 wanahamia New Zealand ambayo ni tayari kuwapokea pia wengine itakapokuwa lazima. Kuna mipango ya kuwapa makazi ya pamoja kwa kusaidia kuhifadhi utamaduni wao.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Tuvalu imekaliwa na watu wa Polynesia tangu zamani (miaka 3,000 hivi iliyopita).

Iliwekwa chini ya usimamizi wa Uingereza katika karne ya 19 kwa jina la "Ellis Islands".

Kati ya 1892 hadi 1916 ilikuwa eneo lindwa na baadaye sehemu ya koloni la Gilbert and Ellice Islands hadi 1974.

Mwaka ule wenyeji walipigia kura pendekezo la kuwa pekee, mbali na visiwa vya Gilbert vilivyokuwa Kiribati baadaye. Tuvalu ikapata uhuru wake mwaka 1978.

Lugha na dini

[hariri | hariri chanzo]

Kuna lugha tatu tu ambazo huzungumzwa nchini Tuvalu, yaani Kiingereza, Kituvalu na Kikiribati.

Upande wa dini, karibu wakazi wote ni Waprotestanti (97%).

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]


Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.