Papa Martin I
Papa Martin I alikuwa Papa kuanzia tarehe 5 Julai 649 hadi kifodini chake tarehe 16 Septemba 655[1]. Alitokea Todi, Umbria, Italia[2].
Alimfuata Papa Theodor I akafuatwa na Papa Eugenio I.
Baada ya kuwa balozi wa Papa Theodori I huko Konstantinopoli, alichaguliwa kuwa mwandamizi wake bila kibali cha kaisari wa Dola la Roma Mashariki.
Kwa kuwa katika Mtaguso wa Laterano (649) na baada yake alipinga uzushi ulioungwa mkono na kaisari Konstans II, wa kwamba Yesu alikuwa na utashi wa Kimungu tu, bila ule wa kibinadamu, hatimaye katika kanisa kuu la Roma akakamatwa na kupelekwa Konstantinopoli kama mfungwa, halafu uhamishoni sehemu za Ukraina kusini, alipofariki baada ya miaka miwili ya mateso[3].
Ndiyo sababu tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake ni tarehe 13 Aprili[4].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
- Orodha ya Mapapa
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
- ↑ https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
- ↑ Norwich, John J. (1988). Byzantium: The Early Centuries. London: Penguin. ku. 317–8. ISBN 0-670-80251-4.
- ↑ Martyrologium Romanum
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Bury, John Bagnell (2005). History of the Later Roman Empire Vols. I & II. London: Macmillan & Co., Ltd. ISBN 978-1402183683.
- Ekonomou, Andrew J. (2007). Byzantine Rome and the Greek Popes: Eastern influences on Rome and the papacy from Gregory the Great to Zacharias, A.D. 590–752. Lexington Books.
- Mershman, Francis (1913). "Pope St. Martin I". Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company.
- Richards, Jeffrey (1979). The Popes and the Papacy in the Early Middle Ages. Routledge & Kegan Paul.
- Siecienski, Anthony Edward (2010). The Filioque: History of a Doctrinal Controversy. Oxford University Press. ISBN 9780195372045.
- West, Charles (2019), '“And how, if you are a Christian, can you hate the emperor?” Reading a Seventh-Century Scandal in Carolingian Francia', ed. Karina Kellermann, Alheydis Plassmann and Christian Schwermann (Bonn, 2019), https://hcommons.org/deposits/item/hc:27953
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Kuhusu Papa Martin I katika Kamusi Elezo ya Kikatoliki
- Pope Saint Martin I in Patron Saints Index Ilihifadhiwa 20 Julai 2008 kwenye Wayback Machine.
- Papa Martino I
- Colonnade Saints in St Peter's Square
Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Papa Martin I kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |