Nafsi ni neno la mkopo kutoka Kiarabu. Linatumika kusisitiza dhati ya mtu (k.mf. "Mimi nafsi yangu"). Hivyo linatumika kutafsiria neno la Kilatini "persona" (kwa Kiingereza "person") ambalo linamtofautisha binadamu (kama kiumbe wa pekee) na wanyama wote na kumpa haki zake za msingi. Tofauti hiyo ilisisitizwa hasa na dini ya Uyahudi iliyomtambua mtu (mwanamume na mwanamke vilevile) kuwa sura na mfano wa Mungu.

Ni msamiati muhimu wa ustaarabu wa Magharibi, unaotumika sana katika saikolojia, sheria, falsafa, teolojia n.k. Maendeleo makubwa katika kuuelewa yalipatikana wakati wa mabishano ndani ya Ukristo kuhusu fumbo la Yesu na Utatu.