Meriba (kwa Kiebrania מְרִיבָה, Meribah, "masutano") ni kituo kimojawapo cha safari ya Waisraeli kutoka Misri hadi Kanaani chini ya Musa ambayo inasimuliwa kirefu na Torati (Kut 17:7; Hes 20:13). [1]

Musa akitokeza maji kutoka mwambani.

Katika Kutoka (Biblia), Meriba inatajwa pia kama Masa, ingawa madondoo mengine yanadokeza kwamba ni mahali tofauti (k.mf. Kumb 33:8)[2][3]

Inaonekana huko Waisraeli walimlalamikia kiongozi wao na hivyo Mungu pia kuhusu maji waliyoyakosa kwa ajili yao na ya mifugo yao. Kwa sababu hiyo, imechukuliwa kama kielelezo cha kumjaribu Mungu kwa utovu wa imani, hasa kwa kuwa kweli maji yalipatikana kimuujiza kutoka mwambani.

Kadiri ya Hesabu (Biblia) 20:12, hata Musa na kaka yake Haruni walikosa imani huko hata wakaadhibiwa kwa kunyimwa fadhili ya kuingia Nchi ya ahadi.

Kwa sababu hiyo pia, kwanza Zaburi (Biblia) 95, halafu Waraka kwa Waebrania 3-4, vinaonya wote kuwa na imani kila siku, si kumjaribu Mungu.

Kadiri ya Kutoka, mahali ni karibu na Refidim, kituo cha mwisho kabla ya Mlima Sinai, lakini kadiri ya Hesabu ni kaskazini zaidi, karibu na Kadeshi.

Tanbihi

hariri
  1. Numbers:33
  2. Peake's commentary on the Bible
  3. Cheyne and Black, Encyclopedia Biblica
  Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Meriba kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.