Kanisa la Roma
Kanisa la Roma ni hasa jimbo la Kanisa Katoliki lilipo katika mji wa Roma (Italia) na kandokando yake.
Ukristo ulifikia huko mwaka uleule wa kifo na ufufuko wa Yesu (kadiri ya imani ya wafuasi wake) unaodhaniwa kuwa 30 BK.
Kadiri ya Matendo ya Mitume sura ya 2, baadhi ya watu ambao siku ya Pentekoste ya mwaka huo walisikilizwa hotuba za Mtume Petro na wenzake wakabatizwa walikuwa wametokea Roma.
Baadaye Mtume Paulo aliliandikia barua yake ndefu kuliko zote, na hatimaye alifanya utume wake huko kwa miaka kadhaa, hata alipouawa (64-67) katika dhuluma ya Kaisari Nero iliyomuua pia Petro huko Vatikani.
Kutokana na kifodini hicho, Wakatoliki wanasadiki Kanisa la Roma limeachiwa mamlaka ya mkuu wa mitume, hivi kwamba askofu wa Roma (yaani Papa) ni mkuu wa maaskofu wote duniani.
Takwimu
haririMwisho wa mwaka 2014 Wakatoliki wa jimbo walikuwa 2,365,923 kati ya wananchi 2,885,272, yaani 82%. Mapadri wanajimbo ni 1.574 na wale watawa ni 3.260, jumla 4,834. Hivi kila mmojawao anapaswa kuhudumia Wakristo 489.
Mashemasi wa kudumu ni 122.
Watawa wa kiume wasio makleri ni 4,952 na wale wa kike 22,775.
Parokia ni 332.