Ilias au Iliadi (kwa Kigiriki Ἰλιάς, ilias, jina mbadala la mji wa Troia) ni utenzi wa kale na mfano wa kwanza wa fasihi andishi ya utamaduni wa Ugiriki ya Kale. Ilitungwa kama utenzi wa fasihi simulizi na kuandikwa mnamo karne ya 8 KK ikiwa na nyimbo au sehemu kubwa 24.

Achilles anamsaidia Patroklos mjeruhiwa
Aya ya kwanza ya Iliadi
Ramani ya Ugiriki ya Kale zamani za Homer

Utenzi huu unasimulia matukio ya vita ya Troia pamoja na habari za mashujaa wake pande mbili za vita hii. Inakusanya pia habari nyingi za miungu ya Ugiriki.

Anayetajwa kama mwandishi ni mshairi Homer hata kama wataalamu wa kisasa wanajadiliana huyu alikuwa nani na kama aliishi kweli.

Katika historia ndefu ya miaka 10 ya vita ya Troia Ilias inasimulia wiki za mwisho tu. Inaanza na hasira ya mungu Apollon kwa sababu ya tendo la Achilles kumteka binti wa kuhani wa mungu huyu na fitina kati ya shujaa Achilles na mfalme Agamemnon inayofuata. Kutokana na fitina hii Achilles anagoma kushiriki tena katika vita na sasa Wagiriki hawawezi kushindana tena na Watroya. Wakati Wagiriki wanaelekea kushindwa Achilles anarudi vitani baada ya kuuawa kwa rafiki yake Patroklos kwa mkono wa shujaa Mtroia Hektor. Anamwua Hektor na kuacha maiti yake kwa siku 12 kwenye mchanga. Mwishoni anatulia na kumruhusu baba yake Hektor kumzika mwanawe.

Majina muhimu katika Ilias ni pamoja na Achilles, Odiseo, Agamemnon, Menelao, Priamo, Hektor, Paris na Helena.

Pamoja na utenzi mwingine wa Homer unaoitwa Odisei, Ilias ni chanzo cha fasihi ya Ugiriki ya Kale.

Viungo va nje

hariri