Nenda kwa yaliyomo

Kiazi kitamu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Viazi vitamu)
Kiazi kitamu
(Ipomoea batatas)
Kiazi kitamu kinachotoa ua
Kiazi kitamu kinachotoa ua
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
(bila tabaka): Asterids (Mimea kama alizeti)
Oda: Solanales (Mimea kama mnavu)
Familia: Convolvulaceae (Mimea iliyo na mnasaba na kiazi kitamu)
Jenasi: Ipomoea
L.
Spishi: I. batatas
(L.) Lam.

Kiazi kitamu (Ipomoea batatas) ni mmea wa chakula uliomo katika familia ya Convolvulaceae. Kuna aina mbalimbali, k.m.:

  • halitumwa - aina njano
  • kindoro - aina nyekundu
  • kirehana
  • sena - aina nyeupe

Chakula ni kiazi au sehemu nene za mizizi yake yenye wanga, vitamini na madini.

Majani mabichi (k.m. matembele, miriba, mitolilo) huliwa pia kama mboga.

Katika Afrika ya Mashariki huliwa pia kama mchembe (vipandevipande vilivyokaushwa katika hali mbichi) au mbute (vilivyokaushwa baada ya kupikwa).

Viazi vitamu hulimwa kote duniani katika nchi za joto kiasi penye maji ya kutosha.

Asili ya mmea iko Amerika ya Kusini na nchini Peru mabaki ya viazi vitamu vyenye umri wa miaka 10,000 yamepatikana. [1]

Kila mwaka takriban tani milioni 103 zinavunwa na hii inaweka Ipomea batatas kwenye nafasi ya tatu ya mimea ya viazi baada ya kiazi cha kizungu na muhogo.

Nchi yenye mavuno makubwa duniani ni China (tani milioni 70.5) ikifuatwa na Tanzania na Nigeria (kila moja takriban tani milioni 3.5). [2]

Picha za aina za Viazi Vitamu

[hariri | hariri chanzo]
  1. Steingold, Alison Clare. "The Uber Tuber," Hana Hou! Vol. 11, No. 4, p. 2 (August/September 2008); retrieved 2012-1-6.
  2. [http://web.archive.org/20161019111658/http://faostat3.fao.org/download/Q/QC/E Ilihifadhiwa 19 Oktoba 2016 kwenye Wayback Machine. Taarifa ya FAO]