Nenda kwa yaliyomo

Pogromu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pogromu dhidi ya Wayahudi huko Lviv mwaka 1941.

Pogromu (kutoka Kirusi погромить, pogromit - kuharibu vikali, kufanya fujo) ni ghasia kali inayolengwa dhidi ya kundi maalumu kama vile wafuasi wa dini au kabila fulani.

Neno latokana na ghasia za fujo katika Urusi wa karne ya 19 ambako Wayahudi walishambuliwa, maduka na nyumba zao kuharibiwa na idadi ya watu kuuawa hovyo. Kwa hiyo neno "pogromu" lataja hasa mashambulio dhidi ya Wayahudi katika Ulaya. Lakini inatumiwa pia kwa mashambulio dhidi ya vikundi vingine.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Pogromu kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.