Nenda kwa yaliyomo

Marudio (fizikia)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Marudio)
Idadi ya mawimbi yanayopita katika dakika ni kipimo cha marudio
Mfano wa taa inayowaka kwa marudio ya a) , b) na c) .. f ni alama ya Hz katika fomula; 1 Hz inamaanisha ya kwamba taa inawaka mara 1 kila sekunde. 0.5 Hz inamaanisha inawaka kila sekunde 2 = mara 0.5 kila sekunde 2; 2 Hz inawaka mara 2 kila sekunde.
T (alama ya tempus, time) ni alama ya wakati katika fomula, inataja kipindi cha marudio yaani ni sekunde ngapi kutoka kuwaka hadi kuwaka.

Marudio (ing. frequency, alama yake ni f) ni kipimo kichachosema ni mara ngapi tukio linatokea tena na tena kila baada ya kipindi fulani.

Kwa mfano ukikaa kando la bwawa au bahari penye mawimbi unaweza kuhesabu ni mawimbi mangapi yanayopita kwako katika dakika moja. Namba hii ni marudio ya mawimbi haya.

Kipimo cha SI kwa marudio ni Hezi (alama Hz).

Marudio katika mazingira yetu

[hariri | hariri chanzo]

Vitu vingi katika dunia hutokea kwa marudio maalumu. Kutambua marudio ya mawimbi ya nuru, sauti, mawimbi ya sumakuumeme na kadhalika kumekuwa msingi kwa sehemu kubwa ya teknolojia tunayotumia, kuanzia redio, televisheni hadi simu na kompyuta.

Kwa hiyo marudio ni kipimo muhimu sana katika sayansi na teknolojia ya kisasa.

Marudio yanaweza kutajwa kwa matukio yote ambayo yanatokea mara kwa mara kufuatana na mfumo maalumu.

  • Marudio ya badiliko la mchana na usiku ni
  • Moyo wa binadamu ina mapigo 50-90 kila dakika hii inalingana na marudio ya 0.83–1.5 Hz).
  • katika bendi au okestra wapiganaji wote wanahitaji kupanga ala zao kwa sauti ya marudio yaleyale, mara nyingi kwa 440 Hz.
  • Sikio la kibinadamu hutambua sauti zenye marudio baina ya 20 Hz na 20.000 Hz, ilhali kiwango cha juu hupungua kuluingana na kuzidi kwa umri wa msikiliziaji.
  • Jicho la kibinadamu huona nuru kati ya 400 THz na 750 THz (terahezi).
  • Mawimbi ya sumakuumeme (ing. electromagnetic waves) hutumiwa kwa mawasiliano kwa redio au simu bila waya kuanzia 100 kHz na GHz kadhaa.


Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Simple English Wiktionary
Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina dictionary definitions (word meanings):