Kucha wa Afrika
Kucha wa Afrika ni ndege wadogo ambao zamani waliainishwa katika Sylviidae, familia ya kucha wengine. Sasa wataalamu wanakubaliana kwamba ndege hawa ni kundi lao lenyewe pamoja na vikucha na kolojojo. Kwa hivyo wamepata familia yao Macrosphenidae. Kucha wa Afrika bila vikucha na kolojojo wanafanana na shoro, kuchanyika na kuchamsitu ambao zamani waliainishwa pia katika familia Sylviidae. Wana mkia mrefu kiasi na rangi yao ni kahawia au kahawianyekundu. Wana michirizi mizito kujumuisha “masharubu”, isipokuwa kucha wa Victorin. Vikucha na kolojojo wana mkia mfupi.
Hula wadudu ambao huwatafuta ardhini, chini ya uoto au katika gome la miti. Hulijenga tago lao kwa umbo wa kikombe katika miti au ndani ya uoto mzito, mara nyingi karibu na ardhi. Jike huyataga mayai 2-5.
Spishi za Afrika
[hariri | hariri chanzo]- Achaetops pycnopygius, Kuchamwamba wa Damara (Rockrunner)
- Cryptillas victorini, Kucha wa Victorin (Victorin's Warbler) – lazima iainishwe katika jenasi yake
- Macrosphenus concolor, Kolojojo Kijivu (Grey Longbill)
- Macrosphenus flavicans, Kolojojo Manjano (Yellow Longbill)
- Macrosphenus kempi, Kolojojo wa Kemp (Kemp's Longbill)
- Macrosphenus kretschmeri, Kolojojo wa Kretschmer (Kretschmer's Longbill) – inawezekana kama si kolojojo lakini aina ya korogoto
- Macrosphenus pulitzeri, Kolojojo wa Pulitzer (Pulitzer's Longbill)
- Melocichla mentalis, Kuchakulu (Moustached Grass au African Moustached Warbler]])
- Sphenoeacus afer, Kucha-nyasi (Cape Grassbird)
- Sylvietta brachyura, Kikucha Kaskazi (Northern Crombec)
- Sylvietta denti, Kikucha Tumbo-njano (Lemon-bellied Crombec)
- Sylvietta isabellina, Kikucha Somali (Somali Crombec)
- Sylvietta leucophrys, Kikucha Nyusi-nyeupe ( White-browed Crombec)
- Sylvietta philippae, Kikucha wa Philippa (Philippa's au Somali Short-billed Crombec]])
- Sylvietta rufescens, Kikucha Domo-refu (Long-billed Crombec)
- Sylvietta ruficapilla, Kikucha Utosi-mwekundu (Red-capped Crombec)
- Sylvietta virens, Kikucha Kijani (Green Crombec)
- Sylvietta whytii, Kikucha Uso-mwekundu (Red-faced Crombec)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Kuchamwamba wa Damara
-
Kuchakulu
-
Kucha-nyasi
-
Kikucha kaskazi
-
Kikucha utosi-mwekundu
-
Kikucha domo-refu
-
Kikucha kijani