Nenda kwa yaliyomo

Aswan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Assuan)


Jiji la Aswan
Jiji la Aswan is located in Misri
Jiji la Aswan
Jiji la Aswan

Mahali pa mji wa Aswan katika Misri

Majiranukta: 24°05′20″N 32°53′59″E / 24.08889°N 32.89972°E / 24.08889; 32.89972
Nchi Misri
Mkoa Aswan
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 275,000
Tovuti:  www.aswan.gov.eg
Msikiti mkuu wa Aswan
Kanisa kuu la Kikopti la Aswan

Aswan (kwa Kiarabu أسوان, Aswān, pia Assuan au Assouan) ni mji wa kusini kabisa nchini Misri wenye wakazi 200,000. Ni makao makuu ya mkoa wa Aswan. Imejulikana duniani kutokana na lambo la Aswan ambalo ni ukuta mkubwa unaozuia mwendo wa mto Nile na kusababisha kutokea kwa bwawa la Nasser.

Tangu kutengenezwa kwa lambo hilo, Aswan imekuwa mji wa viwanda kwa sababu umeme unapatikana kwa wingi tangu 1960.

Utalii ni muhimu pia, kwa sababu karibu na Aswan kuna mabaki mengi ya mahekalu na majengo mengine ya enzi za Misri ya Kale.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Zamani mji ulijulikana kwa jina la Syene au Swan au Seveneh. Inatajwa hata katika Biblia. Ilikuwa mji muhimu wa Misri ya kusini na mara nyingi mpaka na madola ya Sudan. Hivyo Mafarao waliweka huko kituo muhimu cha kijeshi kwa karne nyingi.

Aswan ilikuwa muhimu katika historia ya sayansi. Wazee walitambua ya kwamba wakati wa mchana jua liko juu kabisa angani na fimbo halina kivuli katika saa ya adhuhuri. Mtaalamu Mmisri Eratosthenes alianza hapa upimaji wake uliothibitisha ya kuwa dunia si tambarare, bali duara kama mpira.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu maeneo ya Misri bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Aswan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.