Nenda kwa yaliyomo

Wojtek (Dubu)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
The printable version is no longer supported and may have rendering errors. Please update your browser bookmarks and please use the default browser print function instead.
Wojtek akiwa na askari wa Polandi.

Wojtek alikuwa dubu wa kahawia wa Syria (Ursus arctos syriacus) alinunuliwa, kama mtoto mchanga, katika kituo cha reli huko Hamadan, Iran, na askari wa Polandi ambao waliokolewa kutoka Umoja wa Kisovieti. Ili kupata riziki yake na usafiri, aliandikishwa rasmi kama askari wa kawaida, na baadaye akapandishwa cheo na kuwa koplo.[1]

Aliandamana na askari wenzake kwenda Italia, akihudumu katika kikundi cha 22nd Artillery Supply Company. Wakati wa mapigano ya Monte Cassino, nchini Italia mnamo 1944, Wojtek alisaidia kubeba makreti ya risasi na kuwa mashuhuri na kutembelea majemadari na wakuu wa nchi. Baada ya vita, kuachana na Jeshi la Kipolishi, aliishi maisha yake yote huko katika maonesho ya wanyama ya Edinburgh huko Scotland.

Marejeo

  1. https://www.tvp.info/15256579/pomnik-legendarnego-niedzwiedzia-wojtka-stanal-w-krakowie