Pablo Rosario
Mandhari
Pablo Paulino Rosario (alizaliwa 7 Januari 1997) ni mchezaji wa mpira wa miguu wa Uholanzi ambaye anacheza katika klabu ya PSV na timu ya taifa ya Uholanzi kama kiungo.
Kazi ya klabu
Almere City
Mwaka 2014 Rosario alihamia katika klabu ya Almere City FC. Tarehe 7 Agosti 2015 alicheza kwa mara ya kwanza katika timu hiyo katika mechi waliotoka sare 3-3 nyumbani dhidi ya VVV-Venlo.Aliweza kuingia katika dakika ya 59 kama mbadala wa Soufyan Ahannach.
PSV Eindhoven
Tarehe 25 Julai 2016, Pablo Rosario alisaini mkataba wa miaka minne(4) katika klabu PSV Eindhoven iiliyopo Uholanzi.
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Pablo Rosario kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |