Mfonio
Mandhari
Mfonio (Digitaria spp.) | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kicha cha mifonio
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Mfonio ni aina ya nafaka yenye punje ndogo sana (fonio) unaopandwa katika sehemu za Afrika ya Magharibi. Kuna spishi mbili: mfonio mweupe na mfonio mweusi. Nafaka hii hupendwa katika maeneo makavu yenye mvua isiyotabirika, kwa sababu inakomaa ndani ya wiki 6-8 na fonio ni rutubishi sana.
Spishi
- Digitaria exilis, Mfonio mweupe (White fonio)
- Digitaria iburua, Mfonio mweusi (Black fonio)
Kuna spishi nyingine huko Uhindi iliyo na mnasaba na mfonio ambayo inaitwa raishan (D. cruciata var. esculenta).