Mfereji wa Panama
Mandhari
Mfereji wa Panama ni njia ya maji nchini Panama (Amerika ya Kati) kati ya Bahari ya Pasifiki na Bahari ya Atlantiki.
Kabla ya kujengwa kwa mfereji huu meli zote zilipaswa kuvuka ncha ya kusini ya Amerika na mfereji umefupisha safari hii kwa kilomita maelfu.
Kampuni ya Kifaransa ilianza kujenga mfereji tangu 1880 lakini ilishindwa. Serikali ya Marekani iliendeleza kazi na kumaliza mfereji mwaka 1914.
Marekani ilitawala kanda ya mfereji kuanzia 1904 hadi mwaka 1999 kwa kuikodi kutoka nchi ya PAnama. Siku hizi mfereji uko chini ya serikali ya Panama.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |