Nenda kwa yaliyomo

Nawal El Saadawi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 17:33, 13 Oktoba 2023 na InternetArchiveBot (majadiliano | michango) (Rescuing 2 sources and tagging 0 as dead.) #IABot (v2.0.9.5)
(tofauti) ← Pitio lililotangulia | Toleo la sasa (tofauti) | Pitio linalofuata → (tofauti)
Picha ya Nawal El Saadawi mwaka 2012 katika Tahrir Square, Misri, wakati wa maandamano ya wanawake.
Picha ya Nawal El Saadawi mwaka 2012 katika Tahrir Square, Misri, wakati wa maandamano ya wanawake.

Nawal El Saadawi (kwa Kiarabu: نوال السعداوي ; O 4 Oktoba 193121 Machi 2021) alikuwa mwandishi wa habari, mwanaharakati aliyetetea haki za wanawake, daktari na mtaalamu wa magonjwa ya akili kutoka Misri.

Aliandika vitabu vingi juu ya mada ya wanawake katika Uislamu, akizingatia sana mila ya ukeketaji katika jamii yake.[1] Alielezewa kama "mwandishi na mtetezi wa Ulimwengu wa Kiarabu", na kama "mwanamke mkali zaidi wa Misri".[2] [3]Alikuwa mwanzilishi na rais wa Jumuiya ya Mshikamano wa Wanawake wa Kiarabu na mwanzilishi mwenza wa Jumuiya ya Waarabu ya Haki za Kibinadamu.[4][5]

Alitunukiwa digrii za heshima katika mabara matatu. Mnamo 2004 alishinda Tuzo ya Kaskazini-Kusini kutoka Baraza la Uropa. Mnamo mwaka 2005 alishinda Tuzo ya Kimataifa ya Inana nchini Ubelgiji, na mwaka wa 2012 Ofisi ya Kimataifa ya Amani ilimtunuku Tuzo ya Amani ya Seán MacBride ya mwaka 2012.

  1. "The Guardian", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2022-03-16, iliwekwa mnamo 2022-03-18
  2. "Nawal El Saadawi | Biography, Books, & Feminism | Britannica". www.britannica.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-03-18.
  3. "I don't fear death: Egyptian feminist, novelist Nawal El Saadawi". EgyptToday. 2018-05-24. Iliwekwa mnamo 2022-03-18.
  4. "Nawal El Saadawi". Women Inspiring Change (kwa American English). 2015-03-02. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-12-18. Iliwekwa mnamo 2022-03-18.
  5. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-12-18. Iliwekwa mnamo 2022-03-18.