Nenda kwa yaliyomo

Kipindi cha masomo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 20:58, 16 Januari 2021 na InternetArchiveBot (majadiliano | michango) (Rescuing 1 sources and tagging 0 as dead.) #IABot (v2.0.8)
(tofauti) ← Pitio lililotangulia | Toleo la sasa (tofauti) | Pitio linalofuata → (tofauti)
Ukurasa wa breviari ya karne XVII.

Kipindi cha masomo (kwa Kilatini "Officium lectionis") ni kipindi muhimu cha Sala ya Kanisa katika madhehebu mbalimbali ya Ukristo.

Ni sala rasmi ambayo kwa asili inafanyika wakati wa usiku: ama usiku kati ama kabla ya pambazuko ili kumtolea Mungu sifa na dua pamoja na kutafakari Neno lake katika utulivu wa hali ya juu.

Katika utaratibu wa Kanisa la Roma, unaofuatwa na majimbo karibu yote ya Kanisa Katoliki la Kilatini, sehemu kuu za sala hiyo, kati ya utangulizi na baraka ya mwisho, ni utenzi, zaburi tatu (au vipande vitatu vya Zaburi), kiitikizano kifupi, somo refu kutoka Biblia ya Kikristo, kiitikizano kirefu, somo refu kutoka maandishi ya Kikristo (hasa ya Mababu wa Kanisa), kiitikizano kirefu na sala ya kumalizia.

Katika siku muhimu zaidi baada ya masomo na viitikizano kuna utenzi mwingine mrefu, maarufu kwa maneno yake ya kwanza katika Kilatini, "Te Deum".

Wanaopenda kurefusha sala hiyo katika kukesha wanaweza wakaongeza zaburi nyingine tatu (au vipande vitatu vya Zaburi) kati ya masomo hayo mawili, halafu nyimbo tatu kutoka Agano la Kale na somo la Injili.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu: