Nenda kwa yaliyomo

Takumi Minamino

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 13:04, 9 Agosti 2020 na Hamis Sako (majadiliano | michango)
(tofauti) ← Pitio lililotangulia | Toleo la sasa (tofauti) | Pitio linalofuata → (tofauti)
minamino akicheza red bull salzburg dhidi ya austria

Takumi Minamino (kwa Kijapani: 南野 拓実; alizaliwa 16 Januari 1995) ni mchezaji wa soka wa Japani ambaye anacheza kama kiungo mshambuliaji au winga wa klabu ya Uingereza Liverpool F.C. na timu ya taifa ya Japani.

Minamino akiwa mazoezini na Salzburg.

Minamino alianza kazi yake na klabu ya Cerezo Osaka mnamo 2012. Mnamo mwaka 2014 alihamia Klabu ya Red Bull Salzburg ya Austria ambapo alitumia misimu minne kamili. Kufuatia maonyesho ya kuvutia katika klabu alijiunga na Liverpool mnamo 1 Januari 2020.

Cerezo Osaka

[hariri | hariri chanzo]

Minamino alijiunga na timu ya vijana ya Cerezo Osaka akiwa na umri wa miaka 12 na akaendelea kupitia masomo. Wakati akiwa kwenye klabu ya Cerezo, Minamino aliwatazama wachezaji wakubwa kama Shinji Kagawa na kufanya nao mazoezi.

R.B Salzburg

[hariri | hariri chanzo]

Mnamo 7 Januari, 2014 salamu kutoka Salzburg za kumsaini Minamino ziliwafikia Cerezo. Walifanikiwa kumsaini kwa mkataba wa miaka minne hadi Desemba 2018.

Liverpool

[hariri | hariri chanzo]

Mnamo januari 2020 Liverpool ilimsaini Minamino kutoka Salzburg kwa ada ya pauni milioni 7.25. Mkurugenzi wa michezo wa Salzburg Christoph Freund alisema kwamba "Vilabu vikubwa vimekuwa vikimwangalia na kama ningekuwa wao, nisingekuwa na shaka la kumsaini, Minamino yuko tayari kuondoka". Mpaka sasa Minamino ameshacheza mechi moja akiwa Liverpool, Alicheza dhidi ya Everton katika mashindano ya FA cup, Liverpool iliibuka na ushindi wa goli 1-0.

[1]

Timu ya Taifa ya Japani
Mwaka Mechi Magoli
2015 2 0
2016 0 0
2017 0 0
2018 5 4
2019 15 7
Jumla 22 11
  1. Takumi Minamino at National-Football-Teams.com
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Takumi Minamino kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.