Nenda kwa yaliyomo

Hema ya kukutania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 12:56, 18 Machi 2019 na Escarbot (majadiliano | michango) (wikidata interwiki)
(tofauti) ← Pitio lililotangulia | Toleo la sasa (tofauti) | Pitio linalofuata → (tofauti)

Hema ya kukutania (pia: hema takatifu, hema ya kweli) ilikuwa patakatifu pa Wanaisraeli wakati wa matembezi baada ya kupokea amri za Mungu huko mlima Sinai hadi kujengwa kwa hekalu ya Yerusalemu. Habari zake zinajadiliwa katika Uyahudi na Ukristo.

Jina la Kiebrania lilikuwa "mishkan" (משכן "makao") likimaanisha mahali ambapo Mungu mwenyewe alipokaa kati ya watu wake.

Ilikuwa patakatifu pa kubebwa kwa sababu Wanaisraeli walikuwa watu wasio na makazi ya kudumu. Umbo lake lilikuwa hema yenyewe ndani ya uwanja ulioizungusha. Uwanja ulikuwa na fensi ya nje iliyotengenezwa kwa miti, kamba na vitambaa. Maagizo yanayohusu hema hii yanapatikana katika Biblia kwenye kitabu cha Kutoka milango ya 25 - 30.

Hema yenye vyumba viwili

[hariri | hariri chanzo]

Hema yenyewe ilijengwa kufuatana na mpango wa Kutoka 25.9/26.30): Kuta tatu za ubao mwenye ganda la dhahabu zilifunikwa kwa vitambaa; mafuniko ya juu yalikuwa ngozi. Upande wa mbele ulikuwa mlango uliofunikwa kwa pazia.

Chumba ndani ya hema yenye umbo la mraba kilikuw na urefu wa mita 11,5. Chumba cha ndani kiligawanyika kwa pazia katika sehumu mbili za

  • patakatifu penyewe na
  • patakatifu pa patakatifu.

"Patakatifu pa patakatifu" palikuwa na Sanduku la Agano lenye bao za amri. Sehemu ya "Patakatifu" mbele yake ilikuwa na altari ya ufukizo na meza ya mikate iliyopelekwa huko upya kila siku ya Sabato.

Uwanja wa nje

[hariri | hariri chanzo]

Uwanja ulifichwa mbele ya macho ya wapitaji kwa fensi. Fensi ilikuwa na geti upande wa mashariki uliofungwa kwa pazia kama hema yenyewe.

Kifaa muhimu cha sehmu hii kilikuwa altari ya sadaka za kuchomwa iliyotengenezwa kwa ubao uliofunikwa kwa shaba.

Kitangulizi cha hekalu

[hariri | hariri chanzo]

Baada ya kuingia kwa Wanaisraeli katika Kanaani hema ya kukutania ilipata mahali pa kudumu kwenye mlima wa Shilo. Hekalu ya Yerusalemu ilipojengwa sehemu za hema zilipelekwa Yerusalemu na kuwekwa katika hekalu.

Hekalu ilifuata muundo wa hema kwa kugawiwa katika sehemu za uwanja, patakatifu na nyuma yake patakatifu pa patakatifu.