Mkufu
Mandhari
Mkufu ni mapambo yanayovaliwa na watu shingoni. Hutengenezwa mara nyingi kwa metali au kwa kufunga vito, vipande vya kioo cha rangi au lulu kwenye uzi.
Mikufu ilivaliwa tangu kale ni kati ya mapambo ya kanza yaliyogunduliwa na wanaakiolojia.
Kuna desturi kati ya wafuasi wa dini mbalimbali kufunga alama ya dini yao kwenye mkufu, kwa mfano msalaba kwa wakristo, hilali kwa Waislamu au nyota ya Daudi kwa Wayahudi.