Brooke Allison
Brooke Allison | |
---|---|
Jina la kuzaliwa | Brooke Allison |
Amezaliwa | 26 Novemba 1986 |
Asili yake | Fort Worth, Texas, Marekani |
Aina ya muziki | Pop |
Kazi yake | Mwimbaji |
Miaka ya kazi | 2000–hadi leo |
Studio | 2K Sounds/Virgin |
Brooke Allison (amezaliwa tar. 26 Septemba 1986) ni mwimbaji wa muziki wa pop kutoka mjini Fort Worth, Texas, Marekani. Allison alipata kujulikana zaidi baada ya kutoa wimbo wake wa "The Kiss-Off (Goodbye)" kunako mwaka wa 2001.
Wasifu
Mnamo mwaka 2001, Allison akatoa single yake kwanza iitwayo "The Kiss-Off (Goodbye)", na ikabahataika kushika nafasi ya 28 katika chati za Billboard magazine's Hot Singles Sales.
Albamu yake ya kwanza inaitwa Brooke Allison (albamu), ambayo yenyewe ilitoka kunako mwezi Juni katika mwaka wa 2001.
Mnamo mwaka wa 2002, alikuwa na nyimbo nne ikiwemo na ya "Cinderella II: Dreams Come True" ambayo pia ilitumiwa kuwa kama kibwagizo cha filamu iliyo na jina hilohilo la wimbo na ilipata kutumiwa katika Disney's Princess Favorites. Mwaka mmoja baadaye, alipata kuonekana katika uchezi wa mmoja wa Nickelodeon maarufu kama Taina katika sehemu ya "Hujuma".
Muziki
Albamu
- Brooke Allison (2001)
Single
- "The Kiss-Off (Goodbye)" (2001)
Marejeo
Viungo vya nje
- Brooke Allison Ilihifadhiwa 24 Mei 2011 kwenye Wayback Machine. katika VH1.com
- Brooke Allison katika MySpace