Yohane Wall
Padre na mfia imani wa Kikatoliki wa Kiingereza
John Wall, O.F.M. (Preston, 1620 - Worcester 22 Agosti 1679) alikuwa padri wa shirika la Ndugu Wadogo Warekoleti aliyefia imani sahihi ya Kikatoliki huko Uingereza.
Kisha kutekeleza uchungaji kwa siri kwa zaidi ya miaka 20, aliuawa kwa kunyongwa na kuchanwa utumbo baada ya kukamatwa wakati wa kuadhimisha Misa kutokana na dhuluma ya mfalme Charles II[1].
Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu mfiadini. Kwanza alitangazwa mwenye heri na Papa Pius XI mwaka 1929, halafu mtakatifu na Papa Paulo VI tarehe 25 Oktoba 1970.
Tazama pia
haririTanbihi
haririMakala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |