Vanadi
Vanadi ni elementi na metali ya mpito yenye namba atomia 23 na alama V katika mfumo radidia wa elementi. Ni metali laini na wayaikaji yenye rangi ya kifedha-nyeupe inayotokea katika madini na kampaundi mbalimbali.
Vanadi | |
---|---|
Jina la Elementi | Vanadi |
Alama | V |
Namba atomia | 23 |
Mfululizo safu | Metali |
Uzani atomia | 50.9415 |
Valensi | 2, 8, 11, 2 |
Densiti | 6.11 g/cm³ |
Ugumu (Mohs) | 6.7 |
Kiwango cha kuyeyuka | 2183 K (1910 °C) |
Kiwango cha kuchemka | 3680 K (3407 °C) |
Asilimia za ganda la dunia | 0.01 % |
Hali maada | mango |
Inatumiwa kama sehemu za aloi za chumapua mbalimbali inapozuia kutu na kuongeza uwayaikaji wa chumapua. Aloi hizo zinatumiwa kwa vyombo vya kiganga kwa upasuaji, vipuri vya giaboksi, pamoja na titani katika aloi kwa matumizi ndani ya rafadha za injini za ndege.
Vanadi ina pia umuhimu fulani kwa miili ya viumbe ingawa wataalamu hawana uhakika bado vanadi inafanya kazi gani mwilini.
Picha
hariri-
Kipande cha vanadi
-
Chombo cha vanadi