Shimo
ukarasa wa maana wa Wikimedia
Shimo (wingi: mashimo) ni uwazi au nafasi tupu, mara nyingi wa mviringo, katika gimba manga uliotokea au uliochimbwa ardhini kwa makusudi mbalimbali
Mara nyingi hutumiwa kwa kuhifadhi mazingira.
Kuna aina nyingi za mashimo.
- shimo inaweza kutokea kama hitilafu ambako halitakiwi kuwepo, mfano shimo kwenye jino, barabarani, kwenye sufuria
- shimo inaweza kutengenezwa kwa muda mfano shimo kwenye ardhi kwa kupanda mti humo, kuunda msingi mle, kwenye mtambo au jengo kwa kusudi la kuweka hapa skrubu
- mashimo mengine ni lazima; mfano shimo la sauti kwenye ala za muziki kama gitaa, shimo la kuingiza hewa katika boksi la kubeba vifaranga, mashimo kwenye uwanja wa gofu unapotakiwa kufikisha mpira
- wakati mwingine neno "shimo" latumiwa kutaja kitu kisicholingana na ufafanuzi wa shimo mwenyewe, mfano "shimo jeusi" katika astronomia