Rushwa (pia: chai, chauchau, chichiri, chirimiri, hongo, kadhongo, kiinikizo, kilemba, mlungula, mrungura, mvungulio n.k.) ni aina ya mwenendo usio wa uaminifu au usiofaa kwa mtu aliyepewa mamlaka, kumbe anatumia nafasi hiyo ili kupata faida binafsi.

Mfano wa rushwa.
Bango dhidi ya rushwa.

Ufisadi unaweza kuhusisha shughuli nyingi ikiwa ni pamoja na rushwa na udhalimu, ingawa inaweza pia kuhusisha mazoea ambayo ni ya kisheria katika nchi nyingi.

Upande wa serikali, au kisiasa, rushwa hutokea wakati mmiliki wa ofisi au mfanyakazi mwingine wa serikali anafanya kazi rasmi kwa faida binafsi.

Tazama pia

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rushwa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.