Rocky Mountains (Kiing. kwa Milima ya Miamba), kifupi pia "Rockies" ni safu ndefu ya milima katika Amerika ya Kaskazini ambayo ni sehemu ya milima inayofuatana na pwani la Pasifiki kuanzia Alaska hadi Meksiko. Mara nyingi hutazamiwa kuanza katika jimbo la British Columbia upande wa magharibi wa Kanada huelekea kusini hadi jimbo la New Mexico la Marekani. Urefu wa safu hii ni takriban kilomita 4,800. Mara nyingi hata milima ya Alaska na pia ya Meksiko ya kaskazini huhesabiwa kuwa sehemu za nje za Rockies.

Milima ya Miamba
Mahali pa Rocky Mountains yenyewe
Ziwa Moraine katika Rockies za jimbo la Alberta - Kanada

Mlima mrefu ni Mount Elbert katika jimbo la Colorado mwenye kimo cha mita 4,401 juu ya UB. Mlima mkubwa katika Kanada ni Mount Robson wa British Columbia mwenye kimo cha mita 3,954.

Kijiolojia Rockies zimejitokeza kutokana kwa kugongana kwa mabamba ya gandunia yaani bamba la Pasifiki na bamba la Amerika ya Kaskazini. Mshtuko wa kugongana au kusukumana kwa mabamba haya yamekunja uso wa ardhi na kuzaa safu hii ya milima.


Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Rocky Mountains kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.