Nyanda za juu
Nyanda za juu ni maeneo yaliyoinuliwa juu[1] , ama juu ya maeneo yaliyo jirani au kwa kiwango fulani juu ya usawa wa bahari. Kimataifa hakuna ufafanuzi makini ya istilahi hii[2].
Mara nyingi inataja milima midogo au pia tambarare iliyopo mnamo mita 500 juu ya usawa wa bahari; wakati mwingine milima ya juu zaidi huhesabiwa humo, wakati mwingine inatofautishwa na nyanda za juu.
Mifano ya nyanda za juu:
- Nyanda za Juu za Kusini nchini Tanzania
- Nyanda za juu za Ethiopia na Kenya
- Nyanda za Juu za Uskoti
- Nyanda za juu za Tibet