Rufiji (mto)

(Elekezwa kutoka Mto Rufiji)

Rufiji ni mto mkubwa wa Tanzania. Chanzo kiko Tanzania ya kusini-magharibi katika maungano ya matawimto ya mto Kilombero (Ulanga) na mto Luwegu.

Mto Rufiji katika Hifadhi ya Selous

Unafikia Bahari Hindi kwa njia ya delta yake takriban km 200 kusini kwa Dar es Salaam karibu na kisiwa cha Mafia. Urefu wa Rufiji ni takriban km 600.

Tawimto kubwa katika beseni yake ni Ruaha Mkuu.

Mwaka 2005 daraja lilikamilika linalorahisisha usafiri kati ya Dar es Salaam na mikoa ya Lindi na Mtwara.

Historia

hariri
 
Ramani ya bonde la Mto Rufiji

Wataalamu kadhaa huamini ya kwamba mji wa kale ulioitwa Rhapta na kutajwa katika kitabu cha Periplus ya Bahari ya Eritrea ulikuwepo kwenye Delta ya Rufiji.

Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia manowari ya Kijerumani SMS Königsberg ilizamishwa katika delta ya mto.

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Viungo vya nje

hariri