Luís de Camões
Luís Vaz de Camões (1524 – 10 Juni 1580) alikuwa mshairi Mreno anayesifiwa kama mshairi mkubwa katika historia ya Ureno. Alilinganishwa na Homer, Virgil na Dante. Aliandika mashairi kwa Kireno na Kihispania na utenzi mkubwa wa Os Lusíadas yaani safari za mabaharia Wareno walioongozwa na Vasco da Gama wakielekea Uhindi kupitia Rasi ya Tumaini Jema na pwani la Afrika ya Mashariki.[1]
Kuna habari chache juu ya maisha yake. Alikuwa nusu yatima kwa sababu babake alikufa safarini Luis akiwa bado mdogo. Alipata elimu nzuri akafuata masomo kwenye chuo kikuu cha Coimbra. Akiwa na umri wa miaka 25 akajiunga na jeshi la Ureno akahudumia katika Ceuta (Afrika ya Kaskazini) akatumwa kwenda Uhindi. Alikaa Goa kwa miaka baadaye akapewa kazi kwenye kituo cha Kireno cha Macau huko China. 1570 alirudi Lisboa alipotoa maandiko yake akapewa mshahara kutoka mfalme.
Marejeo
hariri- ↑ "The Lusiads". World Digital Library. 1800–1882. Iliwekwa mnamo 2013-09-01.
{{cite web}}
: CS1 maint: date format (link)
Viungo vya Nje
hariri- Luis Vaz de Camões - makala katika kamusi elezo ya kikatoliki