Kipenyo
Kipenyo (ing. diameter) ni mstari ulionyooka unaokatisha katikati ya duara ukigusana na mzingo.
Kwa lugha nyingine kipenyo ni pia umbali kati ya nukta mbili kwenye mzingo wa duara zilizopo kwenye mstari ulionyooka unaopita kwenye kitovu cha duara.
Umbali kati ya kitovu na mzingo wa duara huitwa nusukipenyo (rediasi).